Paul Makonda "Nilitarajia Kungekuwa na Kampeni Kabambe ya Kulaani Wazushi na Waongo Mitandaoni ila...."

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ameeleza kushangazwa na baadhi ya watanzania kuwa wafuasia wa baadhi ya watu ambao, wamekuwa wakisambaza taarifa zisizo na ukweli kwa nia ovu huku wengine wakieendelea kusifiwa.

Makonda ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Baba Keagan, ambapo amesema ni jambo la ajabu kuona watu wanaosambaza uongo, ndiyo watu ambao wanafuatiliwa sana kwenye mitandao.

"Nilitarajia kungekuwa na kampeni kabambe ya kulaani wazushi, waongo na waovu, ila cha ajabu ndiyo kwanza wanasifiwa, mbona tunaendelea kuwafuata kwenye mitandao? Mbona “hatuwaunfollow? tunataka kujifunza nini kutoka kwao?." ameandika Makonda.

"Tanzania tumeshaingia katika hii hatari hivi inawezekanaje mtu anazusha habari mbaya za mwingine hata kumtakia kifo je kikitokea anapata faida gani? inawezekanaje watu kuinuka na kutetea wanaoharibu maadili ya jamii yetu?Taifa tunaelekea wapi?" ameongeza Paul Makonda.

"Nilitarajia kungekuwa na kampeni kabambe ya kulaani wazushi, waongo ila cha ajabu ndio kwanza wanasifiwa. Mbona tunaendelea kuwafuata kwenye mitandao?mbona “hatuwaunfollow?” tunataka kujifunza nini kutoka kwao? au ndiyo unafiki umeota mizizi?" Mhe. Paul Makonda, RC Dar es Salaam

"Kwa miaka mingi dunia imepambana na uchafuzi wa mazingira(Environment Polution), sasa kuna shida kubwa duniani ya uchafuzi wa akili(Mind Polution). Kuna kasi kubwa ya kuharibu akili na fahamu za watu na kuafanya watetee maovu na kuwapenda watu wabaya kuliko wema" RC
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii inataka simu janja..ati jitto anayo techno yake kule twita kamuazima Lema wa chademe na yy amekwenda uvila kuna Musiba. Lemutuz kawapa vidonge vyao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad