RC Makonda aagiza kesho maduka yote Dar yafungwe hadi saa 5 asubuhi, Siku za kujiandikisha Daftari la wapiga kura zaongezwa



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda ameagiza kuwa siku ya kesho Oktoba 14, 2019 maduka yote ndani ya jiji la Dar es salaam yafunguliwe kuanzia saa 5 asubuhi ili kupisha wananchi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusherehekea kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.


Mhe. Paul Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 13, 2019 wakati akizungumzia juu ya zoezi la uandikishaji wa wananchi kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa .

“Kesho Oktoba 14 ni kumbukizi ya miaka 20 tangu Baba wa Taifa atangulie mbele za haki, Kwakuwa kesho ni siku ya mwisho ya kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kuwapata Viongozi wa Serikali za Mitaa, Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kukuza Demokrasia ndani ya Mkoa wetu naelekeza maduka yote yafunguliwe kuanzia saa 5 asubuhi hapa Dar, Kwakuwa hii ni sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa“, amesema Makonda.

Kesho Tanzania kutakuwa na tukio kubwa la kitaifa la kumbukizi ya miaka 20 ya Mwalimu Nyerere.

Kwa upande mwingine, Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameongeza siku tatu za uandikishaji kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura, uandikishaji sasa utakamilika, Oktoba 17, 2019, badala ya Oktoba 14 ili kuwapa fursa wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad