Polisi TanzaniaYatuma Ujumbe wa Kutisha Yanga

SELEMAN Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa hasira zake za kupoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting zinaelekea kwa Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa anatambua ugumu wa kupambana na timu ya Yanga kutokana na mabadiliko waliyoyafanya ila hesabu zake ni pointi tatu.

“Natambua kwamba Yanga imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ina hasira ya kupoteza isisahau kwamba nasi tumepoteza mchezo wetu wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting tena kwa kujifunga wenyewe bahati mbaya na tuliwadhibiti wapinzani wetu.

“Maandalizi yetu yapo sawa na dozi kwa vijana inaendelea, historia yangu ya kushinda mbele ya Yanga hiyo naachana nayo kwani mpira hatuzungumzii wakati uliopita tunazungumzia dakika tisini, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Polisi Tanzania inatarajia kucheza na Yanga, kesho, Uwanja wa Uhuru, ina pointi tatu ilizozibeba mbele ya Coastal Union kwenye uwanja wa Ushirika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad