Amemwapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Ali Sakila kuwa Balozi
Rais Magufuli amesema “Muende mkawatumikie Watanzania bila kumuonea mtu kwa kadri Mungu wenu atakavyowaongoza. Kazi ya uongozi ni kusimamamia haki kufuata sheria bila kumuonea mtu yeyote”
Aidha, amesisitiza “Unaweza kusemwa vibaya ila wewe endelea na kazi. Si wote watakupenda ila tufanye kazi. Kwa ujumla nawashukuru wote, Mama Samia na kila mtu katika Utumishi wenu”