Rais wa FIFA asikitishwa na mechi iliyochezwa bila mashabiki


Taarifa inayosambaa na kushangaza wengi katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni kuhusiana na ya mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022 iliyokuwa inazikutanisha Korea Kusini na Kaskazini.

Mchezo huo ulikuwa wa kushangaza na kipekee kutokana na kuyakutanisha mataifa mahasimu kihistoria, mchezo huo ulichezwa Jumanne hii katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang bila uwepo wa shabiki yoyote wala vyombo vya habari hususani vya kigeni zaidi ya Rais wa FIFA Gianni Infantino na kumalizika kwa sare ya 0-0.

Infantino ambaye alikuwepo uwanjani, baada ya mchezo alisema kuwa amesikitishwa na kushangazwa mashabiki kutokuwepo uwanjani.

Hakuna chombo cha habari cha kigeni kilichoruhusiwa kuingia uwanjani na mechi haikurushwa Mubashara.

Baada ya mchezo nahodha wa Korea Kusini a Son Heung-min alieleza kuwa mchezo huo ulikuwa kama vita kutokana na wachezaji wa Korea Kaskazini kuwachezea rafu za hatari zaidi.

"Ni mechi iliyokuwa ya rafu sana, ya rafu kiasi ninafikiri kwamba kurudi tu (nyumbani) ukiwa hujaumia ni mafanikio makubwa, wachezaji wa Korea Kaskazini walikuwa wamekamia sana" alisema Son Heung-min

Korea Kaskazini baada ya mchezo ilieleza kuwa imetoa DVD ya mechi hiyo ambayo haikuwa LIVE kwa Korea Kusini hivyo wanaweza kwenda kuonesha marudio katika vituo vyao vya TV.

Hata hivyo imeelezwa DVD hiyo haina ubora wa kuweza kuonekana kwenye TV
Mechi yao ya marudiano itachezwa Juni 4 mwakani nchini Korea Kusini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad