Mwanariadha wa Kenya bingwa wa Olimpiki katika mashindano ya marathon, Eliud Kipchoge ametunukiwa tuzo ya kitaifa ya rais uhuru Kenyatta.
Rais Kenyata ambaye anaongoza sherehe za Mashujaa Day mjini Mombasa pwani ya Kenya amemsifu mwanariadha huyo kwa kuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili mjini Vienna.
“tuzo ya mashujaa wote ,waliopita, wasasa na wajao, unamuendea Eliud Kipchoge,”Uhuru, alisema mwisho wa hotuba yake huku tangazo hilo likishangiliwa kwa vifijo.
Kipchoge, hivi karibuni alitangazwa kuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili.
Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindani la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria.
Ushindi huo haukutambuliwa kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kusukuma kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.
Katika hotuba yake kwa taifa rais Kenyatta alitoa wito kwa Wakenya kuiga mfano wa mwanariadha huyo ili kufikia malengo ya kibinafsi na ya kitaifa
Sina nia mbaya na yeyote au jamii yoyote Ile. Ila naamini pamoja na wingi wa mazoezi na kuwekeza zaidi pesa katika michezo huwa kuna kigezo kingine cha gene ya mtu. Nimesikia hata huko Kenya wanariadha wengi hutoka eneo la Nandi nasikia ni karibu Na Ethiopia (sijui jiografia). Ila najua watu wenye gene kama ya Ethiopia wapo wengi Tanzania eneo la mbulu, singida, manyara na pengine dodoma. Kwanini Tanzania isianze mradi maalum na kuwekeza pesa ili kuwaimarisha watoto wadogo kuanzia miaka 5 katika maeneo tajwa. Wahazabe, wambulu, wanyaturu, wataturu, wamasai n. K. Naamini wakisspotiwa vya kutosha Tanzania itatoa mabingwa kama akina filbert bayi, shahanga n. K. Hayo ni maoni yangu tu.
ReplyDelete