Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia kushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele.
Wanye tabia ya kushindwa kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.
Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaaza kupika maadazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi ni kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha.
Ukitaka kuwa mmoja kati ya watu wasiweza kufanikiwa kimaisha, basi jaribu kuishi maisha ya kukata tamaa mapema unapofanya mambo.