Samatta aeleza alivyoguswa na msiba wa Kamwanya

 
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya TP Mazembe ambaye kwasasa anakipiga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji huku pia akiwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametoa salamu za pole kwa timu ya TP Mazembe kufuatia kifo cha Makamu wa Rais.


Katika salam hizo Samatta ameeleza namna kuguswa na msiba huo huku akiweka wazi kuwa yeye pamoja na mashabiki na timu nzima ya TP Mazembe watamkumbuka daima Kwamwanya.

'Salam zangu za rambirambi ziwafikie familia, ndugu, jamaa, marafiki na timu nzima pamoja na mashabiki wote wa klabu yangu ya zamani ya TP Mazembe kwa kumpoteza Makamu wa Rais wa klabu ndugu Mohamed Kamwanya Ilunga', ameandika Samatta.

Aisha Samatta ameongeza, 'Pumzika kwa amani Rais Kamwanya, tutakukumbuka daima'.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, Kamwanya amefariki usiku wa kuamkia leo Oktoba 1, 2019 baada ya kuugua ghafla.

Samatta aliichezea TP Mazembe kuanzia mwaka 2011 hadi 2015, na kufanikiwa kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo klabu bingwa Afrika, pamoja na kuwa mfungaji bora wa Ligi ya mabingwa mwaka 2015, mafanikio yaliyopelekea kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani mwaka huo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad