Ghana, Senegal, Ivory Coast zashindwa kufuzu CHAN 2020
0
October 21, 2019
Ghana, Senegal na Ivory Coast zote zilishindwa kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) 2020 siku ya Jumapili
Ghana ilishindwa kulipiza bao moja iliyofungwa katika mkondo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, na kutoka sare tasa mjini Ouagadougou.
Hii inamanisha kuwa Black Stars hawatashiriki fainali za mashindao hayo ya Cameroon 2020 ambayo yanachezwa na wachezaji wa Afrika katika mataifa waliozaliwa.
Senegal, pia ni timu kubwa iliyoondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penati.
Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijitutumua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.
Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.
Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0.
Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza kumaanisha waliondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .
Siku ya Jumapili pia, Zimbabwe ilijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.
DR Congo iliichapa Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushindi ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.
Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Libya.
Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0.
Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria.
Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN) yatakayoandaliwa na Cameroon:
Cameroon (mwenyeji)
Tanzania
Uganda
Rwanda
Zambia
Namibia
Togo
Morocco
Zimbabwe
DR Congo
Congo
Tunisia
Burkina Faso
Guinea
Niger
Mali
Tags