Steve Nyerere Ashindwa Kupanda Mlima Kilimanjaro ''Mlima Kilimanjaro sio Mlimani City'


Msanii wa Filamu nchini Steven Mengele, maarufu kama Steve Nyerere amesema kuwa kazi ya kupanda mlima Kilimanjaro si kazi rahisi kwakuwa inamtaka mtu kujipanga na kuwa na afya iliyoimara hii ni baada ya yeye kushindwa kufikia kilele cha mlima huo, kupitia kampeni ya Waziri wa Maliasili na Utalii.

Akizungumza leo Oktoba 2, 2019 na EATV&EA Radio Digital ,Steve Nyelele amedai kuwa hofu na presha ndio sababu ya yeye kutoendelea na safari hiyo ya kuzikamilisha Mita 5,895 za mlima Kilimanjaro.

''Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupanda mlima Kilimanjaro ambao kiuhalisia sio Mlimani City ni mlima wa kweli kabisa na mimi ni mtanzania mzalendo hivyo nilitaka nijionee mwenyewe, kiukweli kuna changamoto inabidi mtu ujiandae na nilijitahidi kwa kweli nimeishia Km 11,kuna wakati nilisikia presha, ulimi kutaka kutoka, unasikia pua zinatanuka yaani ni noma'' amesema Steve Nyerere.

Kwa mujibu wa Steve Nyerere, safari ya twenzetu kileleni katika Mlima Kilimanjaro, ilidhamiriwa kukamilishwa na wasanii 25, lakini hadi leo Oktoba 2, 2019 ni wasanii sita pekee waliofanikiwa kukifikia kilele cha mlima huo, akiwemo Ebitoke, Dude na Single Mtambalike.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad