Tahadhari Kwa Wazazi Wanaotumia ‘Wipes’ Kuwafuta Watoto Wao

Wapo watu ambao hutumia vitambaa laini vyenye unyevu (wipes) ambavyo vimetengenezwa mahususi kwa matumizi ya kufutia vitu mbalimbali, kuwafuta watoto wadogo.

Wipes hizo hutumika kuwafuta watoto wanapokuwa wamechafuka, au wakimaliza kula au wengine huzitumia watoto wanapokuwa wamejisaidia.

Hatahivyo utafiti mpya wa nchini Uingereza unaonesha kuwa wipes hizo au kuwafuta watoto kwa maji ya sabuni bila kuwasuuza na maji safi yasiyo na sabuni, huwasababishia allergy za chakula na kuharibu ngozi zao.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Northwestern kimegundua kuwa ngozi za watoto huwa na aina ya mafuta ambayo huharibiwa na sabuni au kemikali za sabuni zinazopatikana kwenye wipes.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad