Tembo na Almasi Kuamua uchaguzi mkuu wa Botswana


Botswana inapiga kura katika uchaguzi mkuu hii leo na kama BBC ilivyogundua katika mjadala iliouandaa hivi karibuni huko Gaborone, almasi na tembo a u ndovu wana jukumu kubwa katika kubaini mshindi.

Chama tawala nchini Botswana Democratic Party (BDP) kimeshinda kila uchaguzi nchini Botswana tangu uhuru mnamo 1966, lakini mwaka huu kuna uwezekano hilo likabadilika.

Vyama vitatu ya upinzani vimeungana chini ya Umbrella for Democratic Change (UDC).

Wana manifesto walioinadi kwa makini inayoahidi nafasi laki moja za ajira. Katika nchi ambayo zaidi ya 20% ya idadi ya watu hawana ajira, na ambako kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu "wapatao kipato", hilo ni pendekezo la kuvutia.

Makamu rais wa muungano huo wa UDC Dumelang Saleshando ameiambia BBC katika mjadala huo kwamba "ni kuhusu uchumi uliowatenga raia wake".

"Unapoangaliwa sekta ya ujenzi, ni sekta iliokithiri Wachina. Unapotazama sekta ya biashara, Wahindi wamekithiri… hakuna sekta ya kiwanda hata moja nchini iliokithiri raia wa Botswana isipokuwa sekta ya biashara ndogo."

Taifa lililojengwa kwa Almasi

Mara nyingi Botswana hutajwa kuwa hadithi ya ufanisi Afrika uhuru wake ulipatikana pasi kushuhudiwa umwagikaji damu kama ulivyoshuhudiwa katika maatifa jirani zake, haijawahi kushuhudia vita vya kiraia na mara nyingi uchaguzi mkuu haukumbwi na ghasia.

Sehemu ya utajiri wa Botswana unatokana na almasi. Licha ya kwamba Urusi ina almasi nyingi zaidi kwa jumla, machimbo manne ya madini katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya vito vya thamani duniani na Botswana ina hisa zake katika sekta hiyo ya 50-50 na De Beers, inayojieleza kuwa "kampuni inayoongoza duniani ya almasi".

Mkataba huo ulichangia $3.5bn katika mapato ya serikali mwaka jana, na biashara hiyo inawakilisha 40% ya uchumi wa nchi.

Fedhahizo zimejenga barabara, shule na hata hospitali lakini baada ya miaka zaidi ya 50 watu wengi wameanza kufikira pengine wanastahili kupata zaidi kutokana na bahati hiyo nzuri.

Mwaka huu, uvumi kuhusu ufisadi umechangia kuongezeka shaka kuhusu uhusiano huo.

Ushirikiano na De Beers unatarajiwa kuidhinishwa upya mwakani na limekuwa suala kubwa katika uchaguzi huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad