Trump aiomba China kumchunguza mpinzani wake
0
October 04, 2019
Rais wa Marekani Donald Trump ambaye tayari anakabiliwa na shutuma inayoweza kumuondoa madarakani baada ya kumtaka rais wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake Joe Biden, na sasa inasemwa kuwa aliwatakata China wafanye vivyo hivyo.
Aliziambia nchi zote mbili, China na Ukraine kumchunguza bwana Biden ambaye ni kinara wa chama cha Democratic anayetaka kuwania urais, na mtoto wake.
"China inapaswa kuanza kumchunguza Biden," alisema Trump.
Ingawa siku ya alhamisi, rais Trump alidai kuwa madai hayo ni upuuzi.
Katika ujumbe wake wa usiku wa manane kupitia kurasa yake ya Tweeter, Trump aliongeza kuwa yeye ana jukumu la kuchunguza kashfa za rushwa, jambo ambalo linajumuisha na kuuliza na kutoa mapendekezo kwa nchi jirani kutoa msaada.
Trump anamshutumu nini Biden?
Trump anamshutumu bwana Joe Biden na mtoto wake Hunter kwa kashfa za rushwa katika mikataba yao ya kibiashara na kisiasa nchini Ukraine na China , bila ya kutoa ushaidi wa kuthibitisha madai yake.
Wakati ambao Hunter Biden alipoingia katika mkataba wa gesi asilia katika katika kampuni ya Burisma mwaka 2014, maswali mengi yaliibuka kuwa anaweza kuleta mgogoro kisiasa na baba yake.
Ukraine ilikuwa inakabiliana na mgogoro wa kisiasa baada ya kiongozi wake kulazimishwa kuondoka madarakani, huku Biden alikuwa katika ngazi za juu za utawala wa Obama.
Mwaka 2016, Joe Biden aliisukuma serikali ya Ukraini kumfukuza mwendesha mashitaka Viktor Shokin, ambaye ofisi yake ilikuwa inaichunguza kwa karibu mmiliki wa kampuni ya Burisma.
Katika hotuba yake mwaka jana bwana Biden alijisifia kwa kumfukuza bwana Shokin na kutishia kutotoa mkopo wa mamilioni ya fedha kwa Ukraine.
Bwana Trump na washirika wake wanamshutumu bwana Biden kwa kumlinda mwanae.
Hata kama maafisa wengine wa serikali ya Ukraine pia walitaka bwana Shokin kuondoka madarakani kwa sababu ya jitihada zake za kukabiliana na rushwa.
Wiki iliyopita mwendesha mashtaka nchini Ukraini ambaye alichukua wadhifa wa bwana Shokin aliiambi BBC kuwa hakuna ushaidi wa uovu alioufanya bwana Joe au Hunter Biden.
Tags