‘Ugonjwa wa Zari’ Wahamia Kwa Mama Diamond
1
October 23, 2019
ULE ‘ugonjwa’ wa show-off (kujionesha na kuringishia) magari ya kifahari anaodaiwa kuwa nao mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, umehamia kwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama D’.
Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi amekuwa akisifika kwa kutupia picha mitandaoni akipozi na magari makali ikielezwa kuwa huwa analenga kuwarusha roho mahasimu wake.
Sasa ishu hiyo imehamia kwa Mama D au Mama Dangote ambaye naye kwa siku kadhaa amekuwa akitupia picha za magari ya kifahari yanayomilikiwa na familia yake.
Mama Dangote naye inasemekana amekuwa akifanya hivyo kama sehemu ya kuwaziba midomo wanaozusha mambo mengi kuhusu familia yake.
Kwa sasa Mama Dangote siyo yule wa zamani aliyeonekana kutoka familia isiyokuwa vizuri kipesa ambapo sasa ‘anakomoa’ baada ya mwanaye kupata utajiri.
Mama Dangote na Mondi wamekuwa bega kwa bega tangu staa huyo alipoanza kupata umaarufu yapata miaka kumi iliyopita hadi sasa.
Kama ilivyo kwa Zari, maisha bomba ya Mama Dangote yamekuwa yakiibua gumzo huku wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka kumshukuru na kumuomba asife mapema ili aendelee kufaidi vinono vya mwanaye.
Kupitia katika ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote amekuwa akitupia picha na video zikimuonesha akila bata baabkubwa ndani ya jumba la kifahari la mwanaye.
Baadhi ya magari ambayo amekuwa akiyatupia na kuonesha ni kwa kiasi gani mwanaye huyo analaza magari ya mamilioni ya shilingi kwenye maegesho yake ni pamoja na BMW-X6, magari matatu aina ya Toyota Land Cruiser V8, Toyota Noah na Toyota RAV 4.
Kwa upande wake Zari amekuwa akiringishia magari ya kifahari kama Lamborghini Gallardo, BMW-2006, Chrysler-2008, Audi Q7-2010, Hummer H2, Ranger Rover Sports, Toyota Land Cruiser V8 na mengineyo.
Katika ripoti ya Forbes ya mwaka huu, Mondi anatajwa kuwa na utajiri unaofikia shilingi bilioni 11 ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni tatu kutoka shilingi bilioni 8 alizokuwa nazo mwaka jana.
STORI: MWANDISHI WETU, DAR
Tags
Haya Magari ya Anko Shamte.
ReplyDeletepleti namba si zikumbuki ila tulifunga wenyewe sio za Zali.