Ujerumani imesitisha mauzo ya silaha kwa Uturuki baada ya taifa hilo kutuma wanajeshi wake kuvamia wanamgambo wa Kikurdi mashariki mwa Syria,.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas amesema mwaka wa 2018 Ujerumani iliuzia Uturuki silaha za takribani milioni 268 dola za Marekan lakini sasa inaenda kinyume na sheria.
Mapigano kati ya vikosi vya kijeshi vinavyoongozwa na Uturuki na wanamgambo wa Kikurdi yalianza siku ya Jumatano.