Umeme wa Gridi ya TAIFA Kuongeza Mapato


Ujio wa umeme wa Gridi ya Taifa mkoani Katavi wenye uwezo wa kilovolt 132 utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 135 utawezesha kuinua mkoa kiuchumi kutokana na kuokoa gharama kubwa za uendeshaji hasa katika migodi ya dhahabu ambayo inalazimika kutumia gharama kubwa katika ununuzi wa mafuta.

Akizungumza katika ziara ya kikazi ya kutembelea migodi mkoani hapo Meneja wa Shirika la Umeme mkoa wa Katavi, Mhandisi Felix Olang’ amesema kupatikana kwa umeme huo kutawezesha uanzishwaji wa viwanda mbalimbali

NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Ameongeza kuwa mradi huo ukikamilika utasaidia uanzishwaji wa viwanda mbalimbali pamoja na kusaidia wachimbaji wa madini kupunguza gharama za uendeshaji wa mitambo

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Afisa Utawala wa Mgodi wa Katavi na Kapufi Mohamed Twalib amesema wanatumia zaidi ya shilingi milioni mia nane kwa mwezi katika kununua mafuta kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo

Amesema ujio wa umeme wa gridi ya Taifa utawawezesha kuendesha biashara kwa faida ambayo itasaidia kuibua na mambo mengine

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema ujio wa umeme wa gridi ya taifa utasaidia mkoa kuongeza mapato

Pia ametoa wito kwa TANESCO kusimamia mradi huo unaosafirisha umeme kutokea Tabora Ipole Inyonga hadi Mpanda ili uweze kukamilika kwa wakati kwa faida ya watu wa Katavi na Taifa kwa ujumla

“Tutakapokuwa na umeme wa uhakika hata wawekezezaji wataongezeka” alisema Homera

NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad