Unaambiwa..DPP Akusanya Bilioni 3.6, Nyumba 11 Zataifishwa Kutoka kwa Wahujumu Uchumi


SERIKALI kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imeingiza zaidi ya Sh bilioni 3.6 na kutaifisha nyumba sita za washtakiwa waliokuwa wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ndani ya wiki moja.

Hayo yamebainika kutoka na idadi ya watuhumiwa waliokiri makosa Oktoba 4 na Oktoba 7 mpaka 11 mwaka huu katika mahakama hiyo.

Kwa mfano

Oktoba 4, mshtakiwa Yasin Katera aliyekuwa akishtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Takukuru, Godfrey Gugai alilipa faini ya Sh milioni 100 na Serikali ikataifisha nyumba yake moja iliyopo Nyegezi Mwanza.

Alilipa faini hiyo baada ya kukiri kosa la kutakatisha fedha huku akijua fedha hizo ni zao la kuficha ukweli baada ya kudai ni mmiliki wa nyumba wakati nyumba ni mali ya rafiki yake, Gugai.

Mfanyabiashara Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga walikiri makosa ya kutakatisha fedha wakahukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 101 na fedha zao Dola za Marekani 388,000 kutaifishwa na Serikali.

Mahakama iliamuru washtakiwa wakishindwa kulipa fedha hizo wataenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuendesha upatu na wataenda jela miaka 20 kwa kutakatisha fedha.

Oktoba 7-11 wafanyabiashara watatu, Mohammed Yusufali, Arifali Paliwalla na Sameer Khan walilipa fidia Sh 1,201,000,000 baada ya kukiri makosa yao na nyumba nne zilizopo Bagamoyo na Masaki zilitaifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Elinaza Luvanda. DPP aliwapunguzia mashtaka kutoka 544 na kubakia mashtaka matatu.

Akisoma Mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Mkuu Oswald Tibabyekomya alidai, shtaka la kwanza na la pili linamkabili Mshtakiwa Yusufali pekee.

Kwamba katika vipindi tofauti kati ya Januari 2008 hadi Januari 2016 jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Farm Plant Limited, kwa ni
kwa nia ya kukwepa kodi aliwasilisha retuns (marejesho) za kugushi kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha ukwepaji wa kodi wa zaidi ya Sh bilioni 21.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka 2015 hadi Januari mwaka 2016, kwa vitendo kama hivyo, mshtakiwa huyo alisababisha ukwepaji wa kodi wa Sh 1,684,559,546.47
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad