Rais Vladimir Putin wa Russia ameshuhudia majarbio ya makombora matano ya kisasa ya nyuklia katika eneo la Bahari ya Arctic nchini humo ambalo linapakana na Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa, makombora hayo ya nyuklia yamefanyiwa majaribio katika mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo yamefanyika katika eneo zima la Arctic kaskazini mwa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema makombora ya kuvuka mabara yaliyofanyiwa majaribio ni pamoja na RS-24, RSM-50 na Sineva.
Mazoezi ya kijeshi ya Russia yanayofanyika katika eneo la Arctic yanajumuisha wanajeshi 12,000, nyambizi tano za nyuklia, ndege 105 za kivita na magari 213 ya kurusha makombora.
Mazoezi hayo yaliyopewa jina ya Grom-19 au Radi 19 yalikamilika Alhamisi kwa mafanikio.
Wakati akitazama mazoezi hayo kwa njia ya video akiwa mjini Moscow, Rais Putin, akiwa ameandamana na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu amesema majeshi ya Russia yalikuwa yanafanya mazoezi kuhusu vita vya nyuklia na vita vya kawaida.
Mazoezi hayo yamekuja baada ya ya Rais Trump wa Marekani kutangaza kuwa meli za kivita za nchi yake zitaimarisha harakati katika Bahari ya Arctic.