Waarabu Kuamua Hatma ya Young Africans Kimataifa



Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Young Africans wamepangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC ya Misri katika mchezo wa kufuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.

Young Africans itaanzia nyumbani Dar es salaam Oktoba 27, 2019 kabla ya mchezo wa mkondo wa pili Novemba 3, 2019 utakaochezwa nchini Misri. Mshindi wa jumla wa mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi.

Pyramids FC inashiriki michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza, ilianzishwa mwaka 2008, ilifuzu kwa hatua hiyo baada ya kuiing’oa Belouizdad katika raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1.

Klabu hiyo inaongozwa na kocha wa zamani wa Uganda, Mfaransa Sebastien Desabre kuanzia mwezi Julai, baada ya kuvunjiwa mkataba wake wa kukinoa kikosi cha The Cranes, kufuatia kuondolewa mapema katika fainali za Mataifa ya Afrika Misri 2019.

Video: Abdul Maneno ‘Yanga walikosea kumuuza Makambo
Michezo mingine ya hatua hiyo ya mtoano itashuhudia Horoya AC ya Guinea watakuwa na kibarua dhidi ya Bandari ya Kenya, Enyimba (Nigeria) watakuwa wenyeji wa TS Galaxy (Afrika Kusini).

Asante Kototo (Ghana) itacheza dhidi ya FC San Pedro (Ivory Coast), huku Gor Mahia (Kenya) itawakaribisha DC Motema Pembe (DR Congo), UD Songo ya Msumbiji itaivaa Bidvest Wits (Afrika Kusini).

Michezo mingine ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Zamalek (Egypt)/Generation Foot (Senegal) vs ESAE (Benin)

KCCA (Uganda) vs Paradou (Algeria)

Elect Sport (Chad) vs Djoliba (Mali)

Green Eagles (Zambia) vs HUSA (Morocco)

Cano Sports (Equatorial Guinea) vs Zanaco (Zambia)

Fosa Juniors (Madagascar) vs RS Berkane (Morocco)

Cote d’Or (Seychelles) vs Al Masry (Egypt)

ASC Kara (Togo) vs Rangers (Nigeria)

FC Nouadhibou (Mauritania) vs Triangle United (Zimbabwe)

El Nasr (Libya) vs Proline (Uganda)

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad