Waarabu wa Yanga Mmambo Magumu


WAPINZANI wa Yanga, Pyramids FC mambo magumu baada ya juzi kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa pili mfululizo kufuatia kulazimishwa suluhu dhidi ya Smouha.

Huo ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya nchini Misri uliopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni siku chache kabla ya kuvaana na Yanga Oktoba 27, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Pyramids, mchezo uliopita wa ligi ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Al Gaish, licha ya kuendelea kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane.

Wapinzani hao wa Yanga, wameshinda michezo yake miwili ya kwanza dhidi ya ENPPI na Tanta pekee yote iliicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Timu hiyo inatarajiwa kutua nchini wiki hii kuikabili Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano Kombe la Shirikisho ambao utapigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga tayari ipo kambini Mwanza tayari kukabiliana na wapinzani wao hao baada ya kumaliza kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wakati Pyramids ikitoa sare michezo miwili na kushinda miwili, Yanga wenyewe wamecheza michezo mitatu kati ya hiyo wameshinda mmoja na Coastal Union huku wakifungwa mmoja dhidi ya Ruvu Shooting na sare moja dhidi ya Polisi Tanzania.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad