Wadau wa Mtandaoni Wamtolea Povu RC Chalamila kwa Kitendo cha Kuwachapa Wanafunzi



Baadhi wa wadau katika mitandao ya kijamii wamepinga vikali kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kujichukulia sheria na kuanza kuwachapa wanafunzi.

Wadau hao waliandika maoni yao kupitia ukurasa wa Twitter huku wengine wakieleza alikuwa anatumia nguvu kubwa kuwachapa wanafunzi hao.

Wengine walieleza kazi hiyo ya kuwachapa wanafunzi ni bora angewaaachia walimu na yeye RC Chalamila akaendelea na majukumu yake mengine.

Wakili wa kujitegemea Fatma Karume katika ukurasa wake aliandika kuwa huo ni uvunjifu wa sheria. RC haruhusiwi kuwatandika wanafunzi huo ni ukatili na ni kosa la jinai.

Baadhi ya wadau wengine walisema alichokifanya RC Chalamila yupo sahihi kwani wanafunzi hao walitakiwa adhabu zaidi ya hiyo kwani kukutwa na simu shule ni kinyume cha utaratibu.

Jana Chalamila aliwatandika bakora wanafunzi 14 wa shule ya Sekondari ya Kiwanja iliyopo wilayani Chunya baada ya kubaini wanamiliki simu wakiwa shuleni.

Alichukua uamuzi huo baada ya kutembelea shuleni hapo na kupokea taarifa ya shule kutoka kwa Mkuu wa shule kuwa kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanamiliki simu jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

@fatma_karume
#Sikaikimya. Huu ni uvunjifu wa sheria. RC haruhusiwi kuwatandika wanafunzi. Huu ni UKATILI na ni kosa la jinai.

 
@kigogo2014
Yaani RC wa Mbeya anachapa mtoto wangu hivi?! Yaani angekuwa mortuary as we speak na mimi niko jela.. Yaani mtoto kuwa na simu ni kosa? Yaani hawa viongozi ushamba kama bosi wao Meko unawasumbua sana!


Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkuu wa shule, RC wote matatizo. Yaani mkuu wa shule umeshindwa kabisa kudeal na matatizo madogo madogo ya shuleni kwako hadi uripoti kwa mkuu wa mkoa!!? Nawe mkuu wa mkoa uliporipotiwa ulishindwa kabisa kumueleza huyo Mwalimu mipaka kazi yako!!? Kwani hakuna majukumu mengine mkoani hapo hadi wewe RC ukatumia muda wako wa kazi kwenda shule ili kuchapa watoto? Wote wawili ni wa kuwajibishwa

    ReplyDelete
  2. Ila baadhi ya maoni yanajaribu kugeuza tatizo la RC na mkuu wa shule kuwa la kisiasa. Washindwe wote.hayo ni matatizo yao wenyewe kiutendaji. Wahusika wamelisikia na watalishughulikia. Hapa kazi tu. Viva tz.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad