Wakenya Mapokea Miili ya Jamaa na ndugu zao Waliokufa katika ajali ya ndege Ethiopian Airlines


Wakenya wamekusanyika kupokea mabaki ya miili ya wapendwa wao waliokufa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines Familia za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka mjini Addis Ababa mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamekusanyika mjini Nairobi kwa ajili ya kupokea miili ya jamaa zao.

Vipimo vya vinasaba DNA kuoanisha masalia ya watu 157 waliouawa katika ajali hiyo vilifanyika miezi kadhaa iliyopita baada ya ajali.

Watu kutoka nchi 30 walikuwa wamepanda ndege hiyo huku wengi wao wakiwa ni raia wa Kenya.

Zimekuwa ni siku za huzuni kwa familia za Wakenya 32 waliouawa ambapo watapata fursa kwa mara ya kwanza kutazama masalia ya miili ya wapendwa wao.

Mazishi ya faragha yatafanyika leo Jumatatu , lakini haijawa wazi ikiwa masalia hayo yatatolewa kwa familia zao.

Maafisa nchini Ethiopia wanasema miili mingine ambayo bado haijafahamika itazikwa katika kaburi la kumbukumbu litakalowekwa katika eneo la tukio la ajali hiyo.

Awali ndugu na jamaa wa wahanga wa ajali hiyo walilalamikia shirika la Boeing kwa kuchelewa kutoa matokeo ya vinasaba ambayo yangesaidia kutambua miili ya wapendwa wao.

Iliripotiwa kuwa miili ya wahanga wa ajali hiyo ilikuwa imeteketea kiasi cha kutotambulika kwa urahisi.

Wakati huo huo ndugu wa watu waliouawa katika ajali ya ndege aina ya Boeing 737 Max iliyopata ajali nchini Indonesia mwaka jana wamekuwa wakidanganywa ili wasipatiwe fidia, wamesema mawakili wao.

Mawakili wao waliiambia BBC kuwa familia nyingi zilishawishiwa kusaini fomu zinazowazuwia kuchukua hatua za kisheria

Kipindi cha BBC cha Panorama kiligundua kuwa jamaa wengine wa waathiriwa walisaini makubaliano sawa na hayo baada ya ajali nyingine mbili, zilizowazuwia kuishtaki kampuni ya Boeing katika mahakama za Marekani.

Abiria wote 189 na wahudumu wa ndge walikufa wakati ndge ya Boeng 737 Max ilipoanguka baharini dakika 13 tu baada ya kuondoka kutoka katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta tarehe 29 Octoba 2018.

katika kipindi cha wiki kadhaa, ndugu wa waathiriwa walilipewa fidia na mawakili wa kampuni ya bima
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad