Mwanahabari huyo alipandishwa kizimbani kwa madai ya kuongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine, kutokulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya zaidi ya Sh173.24 milioni na utakatishaji wa fedha kiasi cha zaidi ya Sh173.24 milioni.
Wakili Jebra alisema, Kabendera amemuomba radhi Rais Magufuli, akieleza kwamba kama katika utekelezaji wa majukumu yake ya uanahabari kuna eneo alifanya makosa au aliteleza, amsamehe ili awe huru.
“Lakini jambo la msingi, ujumbe wa Erick kwa mheshimiwa rais ni kuwa, kama katika kutimiza wajibu wake kama mwandishi wa habari kuna eneo alikosea au alitereza, tuombe radhi kwa niaba yake, watoto na familia yake kwa ujumla,” amesema Wakili Jebra.
Kauli hii imepokelewa kwa hisia tofauti mitandaoni na huku wengi kuonyeshwa kukasirishwa. Kupitia uwanja wa kutoa maoni wa App ya Opera baada ya habari hii kuchapishwa na haya hapa ni baadhi ya maoni;
Faisali Idd aliandika;
Huyu wakili wa Kabendera sio muungwana. Maelekezo ya Rais: Aombe radhi mwenyewe na arudishe fedha. Huyu wakili kaja na ya kwake. Anahofia akiomba radhi akasamehewa atakosa hela za mteja huyo. Ila ajue Mungu anamuona.
Anaomba radhi au mtoa mada ndie anamuobea?mbona maelekezo yapo wazi tu,siayafuate kama wenzake wafanyavyo sijui kama hizi story za mitandaoni zitamsaidia
Wengine wameenda mbali zaidi na kudai kuwa Wakili Jebra anamharibia Kibendera
Bata Maji aliandika;
Utaratibu uko wazi, hata Kabendera anajua cha kufanya, sasa huyu wakili kaingiaje na zake hapo. Nadhani ana nia ya kumharibia Kabendera na mwisho ataambiwa kakiuka masharti ya msamaha na hapo ndio kutakuwa kilio na kusaga meno.
Na haya hapa baadhi ya maoni mengine;\