Walimu 2 Wasakwa Kwa Kuwapa Mimba Wanafunzi


MKUU wa Mkoa Rukwa, Joachim Wangabo,  ametoa maagizo ya kukamatwa kwa walimu wawili wanaodaiwa kuwapa mimba wanafunzi.
Wangabo alitoa maagizo hayo kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambako amewataka wahakikishe Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mzindakaya, Dastan Mlelwa,  anafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuwabaka na kuwapa mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na tatu.
Wakati huohuo, ameagiza Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mpui anayetuhumiwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo, naye akamatwe.
Rais John Magufuli akiwa katika ziara mkoani humo, alishangazwa na wanaume kutochukuliwa hatua baada ya kuwapa mimba wanafunzi 229 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Rais alisema kuwa kwa taarifa zilizopo, Mkoa wa Rukwa ndiyo unaongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito na akawaasa wanafunzi kuacha ‘kiherehere’ na kujikita kwenye masomo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad