Walioiba Tausi was Ikulu Dar wahukumiwa, Wapewa masharti mazito ya kuishi kwa miezi 6


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Imewahukumu watu watatu kulipa fidia ya Tsh. Milioni 6.8 na kuwaachia huru watu hao, Baada ya kukiri kukutwa na nyara hizo za serikali ikiwamo ndege watatu aina ya tausi.



Hukumu hiyo imesomwa jana Oktoba 30, 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salumu Ally, baada ya washtakiwa kumwandikia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) barua ya kukiri makosa yao.

Kwa upande mwingine, Mahakama hiyo imetaifishwa ndege hao kuwa mali ya serikali. Pia imewaachia huru kwa masharti ya kutokutenda kosa ndani ya miezi sita hii ni baada ya kulipa fidia hiyo.

“Mahakama hii inawaamuru washtakiwa kulipa fidia ya Sh. 6,890,000, ndege hao wanataifishwa kuwa mali ya serikali na inawaachia huru kwa masharti kwamba wasitende kosa la jinai ndani ya miezi sita,” amesema Hakimu Ally wakati akisoma hukumu hiyo.

Washtakiwa hao ambao ni David Graha, Mohammed Hatibu na Mohammed Mahamoud, wote wakazi wa jijini Dar es Salaam, Walidaiwa kujihusisha na genge la uhalifu, kukutwa na nyara za serikali ikiwamo ndege aina ya tausi watatu wa Ikulu ya Tanzania.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa shtaka la kwanza, kati ya Juni Mosi, 2015 na Oktoba 14, mwaka huu waliratibu mipango ya uhalifu kwa kujihusisha na biashara ya ndege hao wenye thamani ya Dola za Marekani 1,500.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad