Baadhi ya wananchi wa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameitikia wito wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya, wa kurudisha noti bandia kwenye vyombo vya dola na kusalimisha takribani noti bandia zenye thamani ya Tsh. 740,000/=.
DC Sabaya jana alithibitisha kupokea fedha hizo kutoka kwa baadhi ya wananchi walioitikia msamaha alioutoa siku nne zilizopita mbele ya maofisa wa Benki Kuu ya (BoT), Kanda ya Arusha.
Mapema wiki hii, Sabaya alitoa saa 72 za kuwataka wenye noti bandia popote walipo wilayani humo, Kuzisalimisha ofisini kwake au kituo kikuu cha polisi Bomang’ombe ili kuepuka kwenda jela.
“Baada ya kufanya mkutano na BoT pamoja na zaidi ya wananchi 850, nilitoa siku tatu nikasema yeyote atakayesalimisha fedha hizo za bandia, baada ya kuonyeshwa tofauti ya fedha halali na bandia ni ipi, mpaka sasa tumeshapokea Sh. 740,000,” Amesema Sabaya.
Kwa mujibu wa DC Ole Sabaya, wahalifu wanaosambaza fedha hizo wanabadilisha Tsh. Mil 1 bandia kwa Tsh. 250, 000 hadi 300, 000 halali.
Wananchi wasalimisha noti bandia za thamani ya 740,000/=
0
October 26, 2019
Tags