Wanaume Wanavyolizwa Kwenye Magroup ya NGONO ya Whats App


DAR ES SALAAM: Dawa ya wanaume wakware wanaopenda ngono na kuchepuka imepatikana kupitia ‘ma-group’ (makundi) ya ngono ya WhatsApp ambayo sasa yamesambaa kwenye mitandao ya kijamii, Gazeti la Ijumaa lina ripoti maalum.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, awali matangazo ya makundi hayo yalikuwa ya kimyakimya na watu walikuwa wakipasiana kulingana na urafiki wa mtu na mtu, lakini sasa mitandao ya kijamii imesheheni.

Mitandao inayoongoza kwa Bongo kutangaza makundi hayo ni Facebook, Instagram na YouTube huku Twitter ikionekana kutawaliwa na ustaarabu fulani kutokana na aina ya watu wanaoutumia ambao wanasemekana ni ‘wale waliokwenda shule’ ambao wanajielewa.

NJIA MPYA YA KIPATO

Katika kutafuta namna ya kujipatia kipato kwa wakati huu ambapo njia zote za ujanjaujanja zimezibwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’, wajanja wachache wamebuni mbinu ya kuwatapeli wananchi kupitia makundi ya mitandao ya kijamii hasa makundi ya WhatsApp.

Katika eneo hili jipya la utapeli mjini, Ijumaa limebaini kuwa kuna wanaume kibao wenye visa tofautitofauti vya kuibiwa kwenye makundi hayo ya ngono ya WhatsApp.

USHUHUDA

Kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao walijikuta wakiingia kwenye mtego huo kutokana na tamaa yake ya ngono, (jina linahifadhiwa) aliwasiliana na mtu kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook ambaye baadaye alimweleza kuwa ana mtandao wa wasichana mastaa na wasio mastaa wanaojiuza na angeweza kuwapata kirahisi kwa kupewa mawasiliano yao na pia kuona picha na baadhi ya video wakiwa watupu kwa kuunganishwa kwenye Group la WhatsApp.

Kwa mujibu wa madai yaliyolifikia dawati la uchunguzi la gazeti hili, vijana wengi wa kiume ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii, wamekuwa wakipigwa vibaya mno mara kwa mara kwa kujiunga katika makundi hayo.

MCHEZO MZIMA

Inaelezwa kuwa, mchezo mzima huanzia Mitandao ya Facebook na Instagram ambapo wengi wa matapeli hao huweka picha za wanawake wazuri wa sura na wenye shepu matata wa Kibongo na kudanganya kuwa wanapatikana kwa njia ya picha na video wakiwa utupu kwenye makundi yao ya WhatsApp huku wakianika namba za simu watumiwe kiasi cha pesa waunganishwe.

Imefahamika kwamba, ‘maadmin’ wa makundi hayo wakishaweka posti hizo katika mitandao hiyo, vijana wengi hasa wa kiume hukimbilia kujiunga kwa kutumia namba zilizowekwa kwenye mitandao hiyo kwa kiingilio cha kiasi cha kuanzia shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa mmoja.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba mtu ukishajiunga kwenye makundi hayo hakuna kinachoendelea na hata ukiwatafuta hawapokei simu.

Katika siku za hivi karibuni ilibainika kuwa, kuna makundi mengi ya WhatsApp yanayoendesha biashara ya ukahaba.

Timu yetu iliingia kubaini kama kweli biashara hiyo inaendelea kwa njia ya mtandao ambapo mmoja wa mapaparazi aliomba kuunganishwa na kundi linalojinadi kuwa, ukitaka kahaba wa kila aina unampata lenye maskani yake Sinza jijini Dar.

Kufuatia paparazzi wetu kutaka aungwe ili apate huduma, alitakiwa kutuma kiingilio cha shilingi 5,000, akatuma na kuomba aunganishwe na mmoja wa warembo wakali waliokuwa wakinadiwa siku hiyo kwenye group hilo.

Heh, imeliwa! Baada ya pesa kutumwa, hakukuwa na mawasiliano tena na simu ikawa haipatikani hewani.

Gazeti la Ijumaa limekusanya visa vingi vya wanaume wa kada mbalimbali waliotapeliwa kwa njia hiyo huku wengine wakiishia kutuma nauli ili mrefu amfuate, lakini hakuna chochote, mwisho wa siku anakuwa ameshatapeliwa.

Ukishaona unaungwa au unashawishiwa kujiunga na kundi ambalo limekaa ‘kihelahela’, akili kumkichwa kwani wengi wamelizwa.

GPL
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad