Katika harakati za kulenga kuvutia wageni zaidi, Saudi Arabia imezidi kulegeza sheria zake kwa sasa mwanaume na mwanamke ambao ni wapenzi na hawajaoana wanaweza kupatiwa chumba kimoja na kulala pamoja katika hoteli lakini hilo ni kwa wageni pekee.
Katika mabadiliko hayo ya sheria ambayo yanaonekana kuendelea katika nchi hiyo inayoendeshwa na sheria za kihafidhina za dini ya Kiislamu sasa ni ruksa hata mwanamke kuchukua chumba katika hoteli jambo ambalo halikuwepo hapo awali.
Hii ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya masharti ya kupata viza yaliyotangazwa hivi karibuni.
“Raia wote wa Saudi wamekuwa wakitakiwa kuonyesha kitgambulisho ama cheti cha ndoa pindi wanapotaka kuchukua chumba cha hoteli. Lakini hili halitahitajika kwa watalii wa kigeni,” hayo yalisemwa na ‘Commission for Tourism and National Heritage’ ya Saudia.NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Falme hiyo inasimamia sheria kali ya dini ya Kiislamu inayokataza mtu kufanya tendo la ngono bila ndoa. Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza nchi hiyo ilitoa ‘visa’ kwa watalii wa kigeni kwa mara ya kwanza bila kuangalia sheria hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wake unaotegemea zaidi mafuta huku maafisa wa Saudia wakipongeza kama hatua kubwa katika historia.
Saudi Arabia pia amefanya mageuzi mengine ya sheria kama vile kuwazuia wanawake kuendesha magari ama kujifunza udereva mwaka 2018 na kuwapatia haki zao pia za kusafiri nje ya nchi.
NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA