Waziri adai haangalii filamu mbovu

 
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza, amewataka wasanii wa filamu nchini kuongeza ubunifu katika kazi zao na kwamba yeye si shabiki wa kazi mbovu za sanaa.


Waziri Shonza amesema kuwa Serikali iko katika harakati za kuboresha soko la filamu nchini kwa kuweka sheria na sera ambazo hazimkandamizi msanii.

“Kikubwa huwa naangalia kazi nzuri, mimi sio shabiki wa kazi mbovu napenda vitu vizuri na napenda filamu , ninachokiona kwa sasa soko la filamu linakuwa ndiyo maana sisi kama Serikali tunafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha tunaendelea kuboresha''. amesema Waziri Shonza.

Aidha Waziri Shonza amewataka wasanii hao, wasisite kumshirikisha kwa jambo lolote ili kwa pamoja waweze kuzitatua changamoto zilizopo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad