Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ametaja viashiria vitatu vinavyosababisha Wakurugenzi wengi kutumbuliwa nchini kuwa ni pamoja na kushindwa kusimamia uwepo wa mahusiano mazuri.
Viashiria kingine ni kushindwa kukusanya mapato na kutosimamia fedha za miradi zinazopelekwa katika maeneo yao ili zifanye kazi iliyokusudiwa .
Akitoa maelekezo ya kazi leo jijini Dodoma kwa wakurugenzi wapya 10 walioteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli,Waziri Jafo amesema viashiria hivyo pamoja na vingine ndio vinasababisha wakurugenzi kuondolewa.
“Wakurugenzi ambao hawana uwezo wa kukusanya mapato ni miongoni mwa indicator kubwa ya wakurugenzi kuondoka,jambo la pili kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo serikali inayopeleka na jambo la tatu ni mahusiano,wakurugenzi mkisikia kila siku boti inapakua inajaza hizi ndio indicator tatu,kwa hiyo hizi parameters tatu nendeni mkazifanyie kazi,
“Siku zote huwa nasema chombo cha Tamisemi ni tofauti na miaka mingine hii ni safari kama umechoka kushika bomba utaachia bomba,na ukiachia bomba ina maana wengine watatamani kushika bomba,nyinyi wakurugenzi kakamateni vizuri bomba,maeneo yote mnakokwenda mnaenda kufnaya replacement kwa sababu maalum,kafenyi kazi,”amesema Jafo.