Waziri Mwakyembe Ashangazwa na Kumwona Maulid Kitenge na Eddo Kumwembe Ndani ya Wasafi Fm "Kule Kwingine sijui Kumebakiwa na nini?"

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe amempongeza msanii wa muziki ambaye pia ni C.E.O wa Wasafi Media, Diamond Platnumz kwa kuanzisha kipindi cha michezo na mchango wake kwenye tasnia ya muziki hapa Tanzania.







Waziri Mwakyembe akiongea leo Jumatatu Oktoba 21, 2019 kwenye uzinduzi wa kipindi cha Sports Arena, Amesema kwa ukubwa wa lebo ya Wasafi, Inahamasisha hata wasanii wachanga kutaka kufikia mafanikio yake.

“Nawashukuru sana Wasafi kwanza kwa kuweka hamasa kwenye muziki. Mtu yeyote anayeingia kwenye muziki sasa hivi anataka niwe kama Diamond ni nzuri hiyo ndio maendeleo. Ndani ya Wasafi kuna Mbosso na wote ni wazuri sana, Leo hapa wameimba wasanii wawili tu, Wana sauti nzuri sana, Mimi nilitaka waendelee kuimba, Nashangaa nyie mmewazoea mnawaangalia tu wakati mimi nilikuwa napiga makofi kama mwendawazimu, Kazi mnayofanya ni nzuri na serikali tunaitambua,” Amesema Mwakyembe na kushangazwa na ujio wa Maulid Kitenge na Eddo Kumwembe ndani ya Wasafi FM.

“Sasa mmeingia kwenye michezo, Sijui niseme nini? Nawashukuru sana. Lakini kuna kitu kikubwa mmekifanya kwa sasa. Kutafuta timu ya wachambuzi nyota wa Tanzania kwenye michezo.  Na kwa kweli ukiangalia hapa unashangaa kule kwingine sijui kumebakiwa na nini? Lakini wapo wasije wakakasirika kuwa oooh! nimewaponda, Hapana kwa kweli nimeangalia Cream nimeiona hapa eeeeh! sijui watakuwa wanatoka toka kusaidia na kule au wapo hapa Full time hapa Wasafi?,“amesema Mwakyembe na kutoa angalizo kwa Diamond.

“Kama ndio hivyo (Diamond) umefanya uchokozi mkubwa, Jiandae kwa mapambano kwani hata kule kumebakia watangazaji.“amemaliza Mwakyembe.

Kauli hiyo ya Mwakyembe imekuja ikiwa ni wiki moja sasa imepita tangu, Wasafi Media kutangaza kuwachukua watangazaji watatu wa kituo cha EFM akiwemo Maulid Kitenge.

Kipindi cha Sports Arena kitaanza kuruka kesho Jumanne Oktoba 22, 2019 kupitia Wasafi FM na kitaongozwa na Watangazaji na wachambuzi mahiri wa soka hapa Tanzania akiwemo Maulid Kitenge na Eddo Kumwembe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad