Wimbi Kubwa la Wanawake Wengi Kuwa na Watoto Bila Kuwa na Baba wa Mtoto

Kumekuwepo na wimbi kubwa kwa hawa dada zetu, kuwa na watoto bila mume.Ukimuuliza anakwambia tumeachana na hawakotayari kuweka wazi sana.

Sasa mimi nashindwa kuelewa tatizo ni sisi wanaume, au ni hawa dada zetu?

Na je mwanaume inakuweje mpaka unafikia hatua ya kumwachia watoto mzazi mwenzio?

Na wewe dada inakuweje uone unaweza muishi na watoto bila mume hata kama hela ya kuwalea unayo?

Yaani jaribuni kuchunguza katika wasichana kumi hapa Bongo, wenye umri 25-35 saba wana watoto na ukiuliza kuhusu baba wa mtoto, au watoto utapewa ngonjera tu!

Tatizo liko wapi? Ebu fungukeni kina dada au sababu ni sisi wanaume?
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tatizo la madada zetu wanapenda pesa, wanajishobokesha kwa wanaume wenye hela. Na haya majamaa yanawapatia kishenzi yani yanawa dunga mimba alafu yana waacha. we tangu lini mwanaume akawa na pesa halafu hana mke. Sasa dawa ya viruka njia ndio hii katulizwe kwanza na mimba na hapo kuolewa ndio asahau kabisa. ila nawahurumia sana lakini hamna namna kama wanataka dezo wapigwe tu.

    ReplyDelete
  2. ni kweli akina dada wengi wapo na watoto bila wazazi wenzao. Kwa mtazamo wangu kwa sababu yamenikuta ni kuwa wanaume wanapenda kuona mwanamke ni chombo chake na anaweza kukitumia atakavyo bila kujali malezi, elimu na kazi waliyofanya wazazi wa binti hadi kufikia yeye kumwona. wanume wanadhani kuwa na mwanamke ni kupata chombo cha kufanya kazi badala ya life partner. hivyo kusababisha misuguano bure.
    Pili, ni uvivu wa kulea wa wanaume na kupenda mteremko maana ukiwa na mimba tu vituko vya kukukatisha tamaaa vinaanza ili tu akwepe jukumu la malezi hasa mwanamke ukiwa safi kifedha.
    Pia udhaifu wa mfumo dume unawaathiri sana wanaume kwa kuwa wanahisi wao wanaweza vyote kuliko wanawake na ikitokea mwanamke anaweza ugomvi na sababu za kitoto huanza jambo linalopelekea wanawake kuchoka na kuvunja mahusiano.
    Aidha,ushamba wa mapenzi ndiyo sababu nyingne, mwanaume kuona siyo lazima kuishi na huyo mzazi mwenzake na pia mwanamke kuona kuwa mbona yeye siyo wa kwanza na anaweza kumpatia malezi motto hata kama baba atazingua.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad