Yanga Watangaziwa Mamilioni Wakiwatoa Pyramids FC
0
October 13, 2019
FITINA zimeanza mapema! Ndiyo kauli unayoweza kuanza nayo kufuatia wapinzani wa Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Pyramids FC kuweka kikao kizito kwa wachezaji wake na kuwaahidi kuwapa donge nono iwapo wataiondosha klabu hiyo na kutinga hatua ya makundi.
Yanga ambao ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), wamepangwa kucheza na Pyramids FC katika mechi za kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya kombe hilo.
Yanga wanaofundishwa na Mkongomani Mwinyi Zahera nao wanajibu mapigo kwa kufanya mipango ya kuandaa fungu la mamilioni ya fedha kwa ajili ya wachezaji wao ili nao wafanye kweli kuanzia katika mechi ya hapa Dar.
Vijana hao wa Jangwani wataanzia nyumbani kwenye mechi itakayopigwa Oktoba 26, Uwanja wa Taifa kabla ya kwenda kurudiana nchini Misri bila ya kuwepo sehemu yake ya kazi kama ambavyo anafanya kwa sasa ambapo yuko nyumbani.
“Mpango uliokuwepo ni kumlipa fedha nusunusu, wahasibu walitaka kumpa milioni 15 kisha baada ya miezi minne tunampa tena milioni 15 na mwisho tunammalizia milioni 10 kwenye mechi ya pili.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, ameliambia Championi Ijumaa kuwa wamepata taarifa hizo za wapinzani wao kukaa kikao baada ya kuwasiliana na mmoja wa watu wake ambao wanaishi nchini Misri ambapo nao wanajipanga kuongea na wadhamini wao kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wachezaji wao.
“Nimeongea na mtu wangu aliye kule Misri na ameniambia kwamba wapinzani wetu Pyramids wameweka kikao na kuweka donge nono mezani kwa wachezaji wao katika mechi hii kuhakikisha kwamba wanatufunga kwenye mechi ya hapa Dar.
“Lakini sisi tumejiandaa kuwamaliza hapa Dar ili tutakapoenda kule Misri tunaenda kumaliza mechi tu. Hapa nyumbani tunataka kupata matokeo mazuri ili ugenini tusiwe na mzigo mzito na badala yake tunaenda kumaliza mechi tu.
“Tumepanga kuongea na wadhamini wetu kama itawezekana kuweka kiasi chochote kuongeza hamasa kwa wachezaji kwa ajili ya mechi lakini hilo amelikataa.
“Hatushindwi kumlipa fedha zake zote kama anavyotaka lakini tuna hofu kwa sababu hadi sasa hayupo eneo lake la kazi na anapokea mshahara, huenda asipate mshahara wa mwezi huu kwa sababu hayupo eneo lake la kazi,” alisema Nugaz.
“Kabla ya mechi hiyo kocha Mwinyi Zahera ameomba mechi mbili za kirafiki ambazo tutacheza na Friends Rangers na Pan African kisha baada ya hapo tutaenda kumaliza Mwanza, Oktoba 24 kucheza na Mbao baada ya hapo tutakuwa tunasubiria mechi hiyo.
“Mechi hizo za kirafiki kocha alizitaka hata kabla hajaenda kwenye timu ya taifa na tutazicheza kwenye viwanja ambavyo havipo wazi ili kumpa nafasi kocha ya kuangalia anachokitaka kwa wachezaji wake.
“Sisi hatuwadharau wenzetu Pyramids hata kidogo licha ya kwamba wana uzoefu mdogo kuliko sisi, pia hatuwaogopi licha ya kufanya uwekezaji mkubwa ndani ya kikosi chao, tutawafanya vibaya hapa Dar watakapokuja,” alimaliza Nugaz.
Katika hatua nyingine Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Wiki ijayo kutakuwa na kikao cha uongozi na matawi mbalimbali kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya timu, kikao hicho kitafanyika hapahapa klabuni.”
Tags