Zifahamu Hatari Kuu Zilizojificha Ndani ya Bafu Lako

Zifahamu Hatari Kuu Zilizojificha Ndani ya Bafu Lako
Watafiti katika nchini Uingereza wanasema kuwa usafi wa bafuni ni jambo linalofaa kuzingatiwa kuliko wengi wanavyodhania.

 "Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu''

"Watu hutumia muda wao katika kusafisha vyoo vyao lakini ingelikuwa vyema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia madawa ya kuuwa bakteria."

1.Kuoga kwa kutumia kifaa cha kukumwagia maji mwilini kwenye bafu za manyunyu

Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini sana, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria.

Hatari nyingine kwa watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho (shower) ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kwenye kifaa hiki ambacho kinaweza kuwa moto sana na kuuchoma mwili.

Msemaji wa kituo cha utafiti Rospa ameiambia BBC: " Tunawaomba watu kuweka maji baridi kwanza ndani ya beseni/ vidimbwi vya maji ya kuoga kwa ajili ya watoto . Kwa kufanya hivyo unawaepusha watoto na hatari ya kuungua kwao wanapojaribu kujifungulia maji ya moto.

Mimea sita ya kushangaza zaidi duniani
"Kuna uwezekano mkubwa kwamba pale unapoweka maji moto kwenye beseni/ama kidimbwi cha maji ya kuoga watoto wanaweza kuyanawa na kuungua, lakini unapoweka maji ya baridi kwanza ndani ya beseni na baadae kuyachanganya na ya moto, uwezekano watoto kuungua utakuwa ni mdogo ".

2. Sabuni ya kuoga huenda ikawa si salama

Mkono ulioshikilia sabuni ya kuogeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kwa kawaida unapotumia kipande cha sabuni cha kuoga unatarajia kitasafisha mikono yako kwa hivyo si rahisi kufikiria kwamba kinaweza kuwa kitovu cha vimelea vya maambukizi.

Hata hivyo unaweza kuwa unajidanganya, kulingana na wataalam wa masuala ya afya.

Profesa wa Oxford anasema: "Bakteria wanaweza kukaa kwenye sabuni ya kuogea na kuhama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine - mfano bakteria aina ya E.coli ambao huishi maeneo hayo.

" Ikiwa mtu atatoka nje ya kikundi cha familia akiwa na bakteria ama mmoja wa familia akipata bakteria hao , basi bafu litakuwa mahala salama kwa bakteria hao kuishi na kusambaa kwa familia nzima."

Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars
Profesa wa Oxford anashauri kuwa matumizi ya sabuni ya maji ni bora kuliko kipande cha sabuni kwa matumizi ya kifamilia .

Na taasisi ya kitaifa ya afya na ushauri bora wa kiafya nchini Uingereza iliwashauri maafisa wa afya nchini humo kutumia sabuni za maji ama zilizowekwa kwenye chupa kunawa mikono .

3. Taulo pia si salama zisipotumiwa kwa makini


'' Usiwahi kamwe kutumia taulo moja na mtu mwingine'' wanashauri wataalam wa masuala ya afya
Taulo iliyokaushwa vizuri na pengine ukaipiga pasi , ni bora kwa kukausha mikono ama uso wako unapokuwa na maji nyakati za mchana.

Lakini usiruhusu kwa namna yoyote ile mtu mwingine aitumie, anashauri Profesa Oxford.

"Taulo ni kitu chenye utata," alisema Profesa Oxford. "Usiwahi kutumia kamwe taulo moja na mtu mwingine - Sishauri hilo."

Asali ''inaweza kukabili maambukizi ya mkojo''
Ni jambo la kawaida kwa watu kutumia taulo moja katika maeneo ya sinki za bafuni/chooni ambayo hutumiwa na wanafamilia na hata marafiki wanaotembelea familia.

Hata hivyo , Profesa Oxford anasema: "Ni heri kuepukika'' . Vimelea vya magonjwa /bakteria vinaweza kukaa kwenye taulo kwa saa nne. Kusema ukweli taulo ni mahala pazuli kwao kukaa kwa sababu hewa imefunikwa na kuwa nzito

"Ningeshauri karatasi laini zitumiwe kama kukausha mikono badala ya taulo na kutupwa kwenye debe la taka au kila mtu awe na taulo yake"

4. Hatari ya kuwaogesha watoto wakiwa na doli zao za plastiki bafuni

Utafiti kuhusu athari za kuingia katika bafu lako na vifaa vingine mfano doli za plastiki unapoenda kuwaogesha watoto wadogo kunaweza kusababisha hatari kubwa.


Gazeti la Times limeripoti juu ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uswiss ya Sayansi na Teknolojia ambapo watafiti walifanyia uchunguzi doli zinazochezewa na watoto wakati wa kuoga na kubaini kuwa asilimia 58 ya doli hizo zilikuwa na bakteria hatari aina ya fangasi.

Mkuu wa utafiti huo alionya watu wasiwarushie watoto wao maji usoni kwa kutumia doli za kuchezea kwani anasema inaweza kusababisha "maambukizi ya macho, maskio au hata ya tumbo".


Doli la plastiki la bata ambalo hutumiwa sana na wazazi kuwapumbaza watoto wakati wanapooshwa ambalo ni mojawapo ya doli zinazoweza kutunza vimelea/bakteria wa maambukizi
5. Kuteleza kwa sakafu ya bafu pia ni hatari nyingine ya bafuni

Ni dhahiri kwamba kuanguka bafuni kuna madhara yake makubwa , sabuni na maji kwa pamoja huifanya sakafu kuwa ya kuteleza.

Mtoto mchanga akiwa ameketi kwenye kiti cha kuogea bafuni. Wataalam wa afya wanasema kifaa kama hiki si salama kwani kinaweza kutunza bakteria wa maambukizi na kumuambukiza mtoto
Watu hupata majeraha ya mara kwa mara kwa kuvunjika mifupa , majeraha ya mwili, na vidonda wanapoingia ama kutoka bafuni , ama wakati mwingine huanguka kwenye sakafu yenye unyevunyevu

Kujaribu kupunguza matatizo haya, watu wanashauriwa kutumia mazulia ya bafuni kwenye sakafu ,mazulia ya kuzuwia kuteleza ndani ya vidimbwi vya maji na kusafisha mabomba na sakafu za bafu mara baada ya kulitumia hususan pale wanapotumia sabundi za mafuta (jeli) ama mafuta ya mwili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad