Zitto Kabwe Afunguka Kuhusu Tetesi Kuhusu Afya ya Rais Magufuli "Ni Busara Serikali Kuwaondoa Hofu Wananchi"


Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano

Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

1. Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumumuni.

2. Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

3. Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini. Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto Zumbli Kambwe, Kama unafikiri faili lako hili ulioambiwa Ni Uamuzi usioludi nyuma Kwenu utaludishwa na Wala usiwe na shaka.

    Kama ni utu..amekufanyia utekelezaji
    wa kuchelewa..ili Ule Posho na Mshaahara kwa kipindi chote. sasa limefika Hapani Mapitio ya Mwisho uhakiki na kupekenyuliwa hala linatinga kwa Ninja halafu Nyumbaniii.

    Pole Dogo..!!! Au utaanzisha Drama ile
    ya kujiteka..?

    Mie huwa sikuelewagi hata nape pia
    roho yako ya Kolosho utapata tabu
    tena sana..!! Mwaya habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Swadakta.
      Anajijua Ubunge hanao na chama kukosa vigezo vyote vinachangia.
      Na twita pia wamemsusa.

      Kwani Uvila mbali?

      Delete
  2. Zitto Zumbli Kambwe, Kama unafikiri faili lako hili ulioambiwa Ni Uamuzi usioludi nyuma Kwenu utaludishwa na Wala usiwe na shaka.

    Kama ni utu..amekufanyia utekelezaji
    wa kuchelewa..ili Ule Posho na Mshaahara kwa kipindi chote. sasa limefika Hapani Mapitio ya Mwisho uhakiki na kupekenyuliwa hala linatinga kwa Ninja halafu Nyumbaniii.

    Pole Dogo..!!! Au utaanzisha Drama ile
    ya kujiteka..?

    Mie huwa sikuelewagi hata nape pia
    roho yako ya Kolosho utapata tabu
    tena sana..!! Mwaya habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete
  3. Zitto Zumbeli Ruyagwa Kambe, Kama unafikiri faili lako hili ulioambiwa Ni Uamuzi usioludi nyuma Kwenu utaludishwa na Wala usiwe na shaka.

    Kama ni utu..amekufanyia utekelezaji
    wa kuchelewa..ili Ule Posho na Mshaahara kwa kipindi chote. sasa limefika Hapani Mapitio ya Mwisho uhakiki na kupekenyuliwa halafu linatinga kwa Ninja halafu Nyumbaniii.

    Pole Dogo..!!! Au utaanzisha Drama ile
    ya kujiteka..?

    Mie huwa sikuelewagi hata nape pia
    roho yako ya Kolosho utapata tabu
    tena sana..!! Mwaya habari ndiyo hiyo.

    Na lile Jiwa la Geita ulilotorosha ni lazima Ulirudishe kwa hiari.

    Ulisha ripoti ostabei kujieezza vp ulitaka kuchukua Ajira ya Dkt Abbasi wakatiwa mkutano wa SADC.

    AU MWITO ADO BADO HAJAKUTAARIFU..??

    ReplyDelete
  4. Teke za Mitandaoni Sasa zimekuwa Karaha

    Huyu Kilaza, alikuwa anatumia Bando ya wiki.Sasa inasemekan kuwa flasi memoli
    yake iliingia maji ndiyo ikaanza kukorapt mafaili huko kwenye uji wa nywele. Hembu wadau hakikini hizi habali mtujuze kuh huyu Dogo.

    Anaendelea kupoteza netiweki..??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad