Acacia yaondolewa Soko la Hisa Dar es Salaam


Kampuni ya Acacia inaondolewa katika orodha ya kampuni zilizopo kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kuanzia leo, Novemba 18, 2019.


Kulia ni Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Emmanuel Nyalali.

Akiongea leo jijini Dar es salaam, Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Emmanuel Nyalali, amesema kampuni hiyo ambayo imedumu katika soko hilo kwa miaka 8 ikiorodheshwa tangu Desemba 2011, ilifutwa katika Soko la Hisa la London Uingereza (LSEG) tangu Septemba mwaka huu, hivyo utaratibu wote umefuatwa.

“Tangu Septemba 2019 Acasia ilikuwa imeshafutwa kwenye soko la Hisa la London (LSEG), ambalo ndio soko lake mama, hivyo taratibu zilikuwa zinamaliziwa tu na Ijumaa iliyopita Bodi ya DSE ilitoa maamuzi hivyo kuanzia leo kampuni hiyo inafutwa kwenye orodha ya makampuni kwenye DSE'', amesema Nyalali.

Awali kampuni hiyo ilikuwa inajulikana kama African Barrick Gold (ABG) kabla ya kubadili jina na kuitwa Acacia Novemba 2014.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad