Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha jela kwa kubaka mtoto wa miaka 8
0
November 08, 2019
Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela mtuhumiwa Addo Aron Nziku baada ya kukutwa na hatia ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 katika kijiji cha kitulila halmashauri ya mji Njombe.
Shauri namba 31 la mwaka 2019, ni kesi iliyomkabili mtuhumiwa Addo Aron Nziku mwenye miaka 26 mbena na mkazi wa kijiji cha matola halmashauri ya mji Njombe, dhidi ya Jamhuri.
Shauri hili likiwa chini ya hakimu James na Mhanusi na Mwendesha mashataka wa serikali Nura Manja ambae ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa anadaiwa kumwingilia mwanafunzi huyo zaidi ya mara tatu kabla ya mtoto huyo kumweleza bibi yake juu ya maswahibu yanayompata.
Mtuhumiwa Addo Nziku anadaiwa kumwingilia kimwili mtoto huyo kwa zaidi ya mara tatu katika eneo la mabanzi yaliyoko nyuma ya nyumba ya wazazi wa mtoto huyo huku mara ya tatu akimuingilia katika eneo la kukata majani ya mifugo ambako mtoto huyo alitumwa kwenda kusaka majani ya simbilisi siku ya tarehe 26 mwezi wa kwanza.
Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kujiridhisha na ushaidi uliotolewa kwa kumkuta na hatia ya kubaka kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili E sambamba na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu namba 16 kama ilivyofanyiawa marejeo mwka 2002.
Tags