Ali Kiba Atangaza Vigezo vya ziara yake


Mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba ametaja mkoa ambao ataanzia kwenye ziara yake ya muziki ambayo itaambatana shughuli za kijamii, afya, michezo, huku akitoa pamoja na vigezo vya msanii atakayepata nafasi ya kuwepo kwenye tamasha hilo.

Alikiba ameiambia EATV & EA Radio Digital, baada ya kutua studio za East Africa Television ambapo amesema ziara yake hiyo inayoitwa Unforgettable Tour, itaanzia mkoani Mwanza siku ya Novemba 29.

"Nilikuwa nataka nikasheherekee birthday yangu, Mwanza ni watu wangu ambao walikuwa wananipa sapoti siku zote, nikifanyaga show vilevile ni mji mzuri sana na mkubwa. Watu wanajielewa wako vizuri na ukiwapelekea burudani ni watu wa nguvu kiukweli", amesema Alikiba.
Akizungumzia vigezo vya msanii kupata nafasi ya kuwepo kwenye tamasha lake, Alikiba amesema, "tamasha ni kwa wale wasanii ambao nimefanya nao kazi ,  kwa hiyo tutakuwa tunatambulisha nyimbo "Live" na msanii fulani aliyefanya kazi na Ali Kiba, kuna wasanii wenzangu ambao wangependa kufanya kazi na mimi siku zote huwa wananisapoti, kwahiyo ratiba itabadilika", ameongeza.

Pia Ali Kiba amesema kuna uwezekano mkubwa  wa kuwepo kwa  suprise ya msanii yeyote kutoka nje ya nchi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad