Aliyemtishia Mwenzake Kumuua kwa Bastola Akamatwa


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema wamemkamata Shabani Hamis Said ambaye anadaiwa kumtishia kwa Bastola dereva wa lori Venance John maeneo ya Mabwe Pande, Oktober 30, 2019 majira saa 3 asubuhi.



Kamanda Taibu baada ya lori la mchanga alilokuwa anaendesha Venance John kukwama bila kupata msaada wa haraka, ndipo akatokea mshtakiwa Shabani Hamis Said akiwa anaendesha gari lake aina ya Subaru na kumtaka dereva huyo ampishe ili apite na akamjibu hawezi kumpisha kwa sababu amekwama katika mchanga.



Baadae wananchi wakatokea na kumpa msaada wa kumkwamua na kuondoka lakini alipofika mbele mshtakiwa alimzuia dereva huyo wa lori na kuanza kumtupia maneno kisha wakaanza kujibizana na kufikia hatua ya mshitakiwa kuamua kutoa Bastola na kutishia kumuua Venance.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad