Antonio Nugaz Ajitetea kwa Staili hii ”Uzuri hazikufika bao 5 kama Majirani zetu, Mrudi tuupambanie Ubingwa wa ligi”
0
November 04, 2019
Msemaji na Afisa Muhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ule msemo wa kila mtu ashinde nyumbani kwake unamaana kubwa sana katika mchezo wa soka, kauli hiyo inajiri baada ya timu hiyo kupoteza nyumbani kwa mabao 2 – 1 dhidi ya Pyramids FC kisha ugenini ikichapwa 3 – 0 michuano ya kombe la Shirikisho.
Mbali na kichapo hicho, Nugaz hakusita kuwachokoza hasimu wao Simba SC kwa kudai pamoja kuwa wamefungwa lakini hazikuwa nyingi kama za majirani zao ambao walipigwa mabao matano (5).
”Mumepambana sana tumeona ila kiukweli ile kila mtu ashinde kwao Ina maana sana. Football tuje sasa tupambanie Ubingwa, uzuri wenyewe hazikufika kama za Majirani zetu goli tano (5) mpaka half time,dah zile zilikuwa nyingi mnooo.” Ameandika Nugaz.
Hata hivyo Msemaji huyo wa Yanga SC anaamini kuwa lipo ambalo wamejifunza baada ya kupoteza michezo yao yote miwili ya nyumbani na ugenini, akigusia hasa katika upande wa uwekezaji wa timu.
Antonio Nugaz ameongeza ”Kiukweli lipo kubwa sana la kujifunza kutokana na kupoteza michezo yetu yote miwili ya nyumbani na ugenini. Uwekezaji kwenye timu yetu, branding kwa upana wa timu yetu.”
”Inabidi tujitathmini haswa kipi na kipi kimetuangusha ili tuweze kujipanga kwa mashindano yajayo na maeneo gani zaidi ya kuyaboresha (kuanzia mfumo, benchi la ufundi mpaka aina ya wachezaji) kwa pamoja ili tucheze mpira wa ushindani kwa ligi ya ndani na hata mashindano ya kimataifa. Siku njema Acha mapambano yaendelee.” Amemalizia.
Yanga SC ilikuwa timu pekee ambayo ilibaki kwenye michuano ya kimataifa baada ya kutolewa klabu bingwa barani Afrika na kudondokea kombe la Shirikisho ambapo hapo jana iliyaaga mashindano hayo kwa tofauti ya mabao 5 – 1 dhidi ya klabu ya Pyramids FC kutoka Misri.
Tags