Asiyemuunga JPM tutakutana mbinguni' - Makonda

 
Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa hadi sasa tayari zimeshatengwa Dola Milioni 120, kwa ajili ya ujenzi wa mto Msimbazi, eneo linalotarajiwa kuwa la kitalii.



Hayo ameyabainisha leo Novemba 4, 2019, alipotembelea mradi wa upanuzi wa barabara za njia nne kutoka Kinondoni Morocco hadi Mwenge, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea ndani ya mkoa huo.

"Mto Msimbazi wenye urefu wa Km 32 tunajenga na pesa zimepatikana Dolla Milioni 120, kuhakikisha kwamba mto huo unatumika kama sehemu ya utalii, jamani hakuna mwingine wa kufananisha kwa zama zetu zaidi ya Rais Dkt John Magufuli, anayetaka amuunge mkono asiyetaka tutakutana naye mbinguni sisi tukiwa tunakula raha yeye yupo upande wa pili anachomwa moto" amesema Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda amewataka wakazi wa Kinondoni, Mtaa wa Bwawani, kuhakikisha wanatunza mifereji mikubwa waliyojengewa kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua na waachane na tabia ya kumwaga taka ili kuwaepusha na athari za kujaa maji na mafuriko katika makazi yao.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad