Baada ya kuachana na Mlela, Ebitoke aliwinda Penzi la Diamond


Msanii wa Vichekesho Ebitoke ameamua kuvunja ukimya na kuonyesha hisia zake za mapenzi kwa Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Ebitoke ambaye siku za hivi karibuni ameachana na aliyekuwa mpenzi wake, Yusuph Mlela ameamua kuweka hisia zake wazi baada ya kwenda kwenye ukurasa ya Instagram ya Diamond Platnumz na kumuandikia ujumbe kuwa anampenda.

"Nakupenda, nikikupata nitafurahi. Siwezi kuficha hisia zangu kwa mtu ninayempenda," alieleza Ebitoke,

Hata hivyo mashabiki wa Diamond walionyesha kukerwa na Kitendo hicho cha Ebitoke na kumsihi aachane na msanii wao.

Haijulikani iwapo jitihada za Ebitoke zitafua dafu kutokana tayari na Diamond Platnumz yupo kwenye mahusiano rasmi na Tanasha Dona kutoka nchini Kenya ambapo wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie sikuamininilivyoona DM.
    Mlela wewe Ulie tuu. Mondi amesha nyapia nyapia ila Ebitoke anaplei haadi gemu. lakini inaelekea ataiachia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tena nasikia Mondi hakosekani katika Anga za Ebi. Hata Madale wanamtafuta saa zingine yuko huku. Mlela umepoteza Mtoto kama alivyo poteza Beni paulo.

      Nyie vipi mnamuachia Domo.

      mtoto badokilomita zinadai.

      Delete
    2. Tena nasikia Mondi hakosekani katika Anga za Ebi. Hata Madale wanamtafuta saa zingine yuko huku. Mlela umepoteza Mtoto kama alivyo poteza Beni paulo.

      Nyie vipi mnamuachia Domo.

      mtoto bado kilomita zinadai.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad