Dk. Bashiru Amcharikia Benard MEMBE...Amtaka Kuacha Kuwa Juu ya Katiba


Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM), DK. Bashiru Ally amempa za uso aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje, Bernard Membe, na kumtaka kuacha kuwa juu katiba ya chama.

Bashiru amemtolea uvivu Membe leo wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV, kupitia chaneli yake ya Youtube.

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika. Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad