Biashara United yamfuta kazi Kocha wao Mkuu


Timu ya Biashara United imetangaza rasmi kuachana na kocha wake Amri Said kwa sababu aliondoka na kuiacha timu ikiwa kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Afisa Habari wa timu hiyo Shomari Binda amesema kuwa wameachana rasmi na mwalimu wao Amri Said na tayari wamemwandikia barua kupitia mwanasheria juu ya uamuzi waliouchukua kama kamati ya utendaji.

"Mwalimu aliondoka kwenye klabu bila ya taarifa rasmi wakati klabu ikiwa kwenye maandalizi ya michezo mbalimbali ya ligi. Tumeona si jambo jema na tumeamua kusitisha mkata wake." alisema.

Hata hivyo taarifa za ndani zinadai kuwa Amri Said aliamua kuiacha timu kutokana na kutolipwa mishahara ya miezi kadhaa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad