Bunge lapitisha wanaoambukizwa Ukimwi kulipwa fidia


Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limefanya marekebisho ya Sheria ya Udhibiti wa Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI, ambapo limeipa Mahakama kutoa amri ya fidia kwa mtu ambaye ameambukizwa VVU kwa makusudi.

Akiwasilisha muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Adelardus Kilangi alisema, marekebisho hayo yanalenga kuainisha wajibu kwa mtu anayejipima VVU na mtu anayetoa au kusambaza vifaa vya kujipima VVU na kumuwezesha Waziri kutoa miongozo ili kuhakikisha kuna usimamizi wa viwango vya vifaa vinavyosambazwa au kuuzwa kwa watumiaji.

Sababu ya mama kumzika mwanaye akiwa hai
Sheria hiyo ipo katika muswada wa sheria ya Marekebisho mbalimbali namba saba wa mwaka 2019 uliowasilishwa na kupitishwa na Bunge Jana Novemba 12, 2019.

Pia, Bunge limepitisha Umri wa Mtoto kujipima VVU kuwa ni miaka ni 15, huku Wabunge wa upinzani wakitaka iwe miaka 12.

Muswada huo pia umependekeza kuweka wajibu wa kutunza siri kwa mtu anayemsaidia mtu mwingine kujipima na kufanya kitendo cha kutoa siri kuwa kosa chini ya Sheria hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad