Bunge Lapitishia Sheria ya Mtu Kujipima Virusi vya UKIMWI Mwenyewe ‘Maambukizi Mapya Yamehamia Kwa Vijana’



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Novemba 12, 2019 limepitisha Sheria inayotoa mamlaka kwa mtu kujipima Virusi vya UKIMWI mwenyewe.



Sheria hiyo, Itaruhusu mtu yeyote kuanzia miaka 15 na kuendelea kujipima mwenyewe jambo ambalo awali lilikuwa linafanyika kwenye vituo vya afya pekee.

Akiongea mapema baada ya bunge kupitisha sheria hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Faustine Ndugulile amesema Sheria hiyo itasadia watu wengi hususani wenye uoga kujipima kwa urahisi.

Ndugulile amesema kuwa kwa sasa kundi linaloongoza kwa maambukizi mapya ya VVU ni vijana ambapo wasichana ndio wanaoongoza kwa asilimia kubwa huku wanaume wakitajwa kuwa kundi linaloongoza kuogopa kupima virusi vya UKIMWI.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad