Burna Boy Azuiwa Kushiriki Matamasha Afrika Kusini...Kisa Kizima Hichi Hapa
0
November 21, 2019
Matamasha mawili yaliyopangwa kumshirikisha mwanamuziki nyota wa Nigeria nchini Afrika Kusini Burna Boy yamefutwa kufuatia "kuongezeka kwa vitisho vya ghasia ", imesema taarifa kutoka kwa waandalizi.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo mwanamuziki huyo ameteuliwa kuwania taji la tuzo za Grammy katika orodha ya albamu bora ya muziki duniani.
Boy alikuwa amepangiwa kucheza muziki wake katika kile kilichoitwa Tamala la Afrika Ungana( Africans Unite concerts ) katika miji ya Cape Town na Pretoria mwishoni mwa juma.
Tangazo kwamba angeonekana kwenye tamasha hili liliibua utata kwani mwezi Disemba wakati kulikuwa na wimbi la ghasia za ubaguzi nchini Afrika kusini , Burna Boy aliapa kutokwenda tena nchini Afrika Kusini hadi serikali ''itakapo amka''
Kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema binafsi alikuwa na ''uzoefu wa ubaguzi mikononi mwa Waafrika Kusini " mnamo mwaka 2017.
Mapema mwezi huu, baada ya kubadili mawazo juu ya kwenda Afrika Kusini, Burna Boy alisema kuwa atatoa msaada wa mapato atakayoyapata katika tamasha kwa waathiriwa wa mashambulio ya ubaguzi:
Lakini mwaliko wa nyota huyo wa muziki wa Afrobeats alikosolewa na baadhi ya wasanii wa Afrika Kusini.
Wiki iliyopita , kikundi kinachojiita Tshwane Entertainment Collective kiliandika barua kwa serikali kuhusiana na tamasha hilo, kwa mujibu wa Times Live.
"Yeyote aliyefikiri kuwa nchi inahitaji shughuli ya mahusiano ya umma ya aina hii angelikuwa amefikiria matokeo mabaya ya upotoshaji na uchochezi usio na kibali uliofanywa na msanii huyu mwenyewe" Collective kilinukuliwa kikisema.
" Hakusambaza tu uongo kupitia ukurasa wake, bali alichochea ghasia na chuki ," iliongeza taarifa hiyo.
Burna Boy, ambaye awali katika ujumbe ambao sasa umefutwa wa Twitter alimtishia msanii wa Afrika AKA, alikanusha kwamba alikuwa anachochea ghasia, na kwamba katika ujumbe wake wa twitter alitoa wito wa umoja:
Ikitangaza kufutwa kwa matamasha hayo, kampuni ya Phambili Media ilisema kuwa ilichukua umamuzi huo baada ya wito wa Tshwane Entertainment Collective wa kuwataka watu kuyasusia na "kongezeka kwa vitisho kutoka kwa makundi mengine ya umma ".Lakini kampuni hiyo haikuelezea wazi vitisho hivyo vilikuwa ni vya aina gani: "Usalama wa wahudhuriaji wote , wananii na wahudumu ni jambo linaloangaliwa kwanza," iliongeza.
Tags