CCM yadai upinzani umekosa vigezo katika uchaguzi wa serikali za mital
0
November 25, 2019
Baada ya vyama 7 vya upinzani nchini Tanzania kususia uchaguzi wa serikali za mitaa, kiongozi wa chama cha upinzani cha TLC (Tanzania Labor Party ) Tanzania Augustino Lyatonga Mrema anasema walichezewa rafu na kufanyiwa figisu.
Bwana Mrema ameiambia BBC kuwa wakala wa chama chake waliondolewa kwenye vituo mbalimbali vya uchaguzi na hivyo chama chake hakikuwa na uwakilishi.
Wapinzani nchini Tanzania wanadai mchakato mzima wa uchaguzi huo uliofanyika Jumapili ulitawaliwa na udanganyifu uliotekelezwa na Chama tawala CCM kwa ushirikiano na maafisa wa uchaguzi.
Hata hivyo katika mahojiano na mwandishi wa BBC Sammy, msemaji wa CCM Bwana Humphrey Polepole ameiambia BBC kuwa wapinzani wameshindwa vigezo na sifa na kukana madai kuwa serikali ina mpango wa kuwaondoa wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao.
Tags