CHADEMA Watangaza Kutoshiriki Uchaguzi Serikali Za Mitaa Kwa Madai ya Kufanyiwa Rafu
0
November 08, 2019
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika November 24, mwaka huu. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo leo kwa madai kuwa uchaguzi huo ni batili na wakishiriki watahalalisha ubatili huo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amatangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema sababu kubwa ni wagombea wa chama hicho kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
Mbowe amesema mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na wabunge, maazimio waliyokubaliana ni kugomea uchaguzi huo sababu majina ya wagombea wengi kukatatwa.
“Sisi kama chama tumeamua hatutashiriki zoezi hili na ninatoa amri kama Mwenyekiti wa viongozi na wagombea nchi nzima wasitishe kugombea na wasitishe kukata rufaa.
“Waachane na kuweka mapingamizi hatupo tayari kubariki ubatili." amesema Mbowe.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.
Tags