Kwa mujibu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, China imezipa jukumu Ofisi mbili la kuendeleza mfumo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano ya simu wa 6G
Wizara hiyo imebainisha kuwa moja ya Ofisi hizo inajumuisha Mawakala wa Serikali wanaowajibika katika utungaji wa sera husika na nyingine inajumuisha Wataalamu 37 watakaowashauri watunga Sera.
Awali, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Wang Xi alisema Ulimwenguni ujuzi kuhusu teknolojia hiyo bado upo katika hatua za majaribio bila kuwepo kwa ufafanuzi wa makubaliano na matumizi yake
Alisema, Wizara itafanya kazi na idara husika kuweka mpango wa maendeleo ya 6G, na itafanyia kazi mafanikio katika nadharia zake za msingi, teknolojia na viwango muhimu.